Tetesi

Richarlison, Sancho kucheza Saudia

TETESI za usajili zinasema fowadi wa Tottenham na Brazil, Richarlison mwenye umri wa miaka 26 na winga wa Manchester United na England, Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 23 huenda wakajiunga na Ligi ya Kulipwa Saudi Arabia Januari 2024. (Telegraph – subscription required)

Juventus pia ina nia kumsajili Sancho lakini kwa dili la mkopo tu na United kulipa sehemu ya mshahara wake.(Fabrizio Romano)

Hata hivyo, United haiko tayari kumwachia Sancho kwa kumruhusu kuondoka wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2024. (Football Insider)

Tottenham inaangalia uwezekano wa kumsajili fowadi wa Juventus na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Samuel Iling-Junior mwenye umri wa miaka 20, Januari 2024.(Independent)

Kiungo mbrazil wa klabu ya Corinthians, Gabriel Moscardo ambaye anawaniwa na Arsenal na Barcelona, amesema Chelsea ilikuwa na nia kumsajili majira yaliyopita ya kiangazi.(Talksport)

Real Madrid imewaongeza katika orodha yake ya usajili kiungo wa Ujerumani, Florian Wirtz, 20, beki wa Uholanzi Jeremie Frimpong,22, na fowadi wa Nigeria, Victor Boniface, 22, wanaokipiga Bayern Leverkusen.(Football Transfers)

Related Articles

Back to top button