Tetesi
Belouizdad yamfungia kazi Aziz KI

DAR ES SALAAM: KIUNGO mshambuliaji ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, Stephen Aziz Ki amewekewa ofa mpya na klabu ya CR Belouizdad ya Algeria.
Barua iliyotolewa na klabu hiyo imeonesha Aziz Ki amepewa ofa ya mshahara wa Sh milioni 97.
Barua hiyo imeonesha CR Belouizdad itampa Ki pesa Sh milioni 291 kwa mkupuo kwa miezi mitatu .
Pia atapewa nyumba kali, gari kali na tiketi mbili za ndege za biashara zenye hadhi kwa mwaka mmoja.
Wakati timu hiyo ikiweka ofa hiyo muda mchache ujao Stephane Aziz Ki ataenda kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu hatma yake ya kusalia au kuwaaga Yanga.