Tetesi

Ten Hag ‘out’ mwisho wa msimu

TETESI za usajili zinasema Manchester United itamtimua kocha wake Erik ten Hag mwisho wa msimu huu. (Football Insider)

Kocha anayeondoka Bayern Munich, Thomas Tuchel ana nia kuchukua mikoba Manchester United.(Telegraph – subscription)

Kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim, kocha wa zamani wa Chelsea na Brighton, Graham Potter na Kocha wa England Gareth Southgate pia wako katika ushindani kuchukua nafasi ya Ten Hag. (inews), (FootMercato)

Jose Mourinho, aliyetimuliwa na Roma Januari, 2024, angependa kurejea Old Trafford lakini Manchester United haitaki kumteua tena. (Manchester Evening News)

Kiungo mreno wa Manchester City, Bernardo Silva, 29, anataka hatma yake itafutiwe ufumbuzi ifikapo mwisho wa michuano ya Kombe la Ulaya(Euro 2024) kufuatia kuendelea kuhusishwa na Barcelona.

Ameripotiwa kuwa na kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 50 katika mkataba wake. (90min)

West Ham imefungua mazungumzo kumsajili winga mbrazili wa Corinthians,19, Wesley Gassova, ambaye ni mlengwa wa usajili wa Liverpool. (Standard)

Newcastle United imefikia makubaliano kumsajili beki wa England anayekipiga Bournemouth, Lloyd Kelly, 25. (Foot Mercado – in French)

Related Articles

Back to top button