Nyumbani

RC Tanga aongoza matembezi ‘Amka na Samia’

TANGA: WANANCHI  wa Mkoa wa Tanga leo wamejitokeza kwa wingi kushiriki matembezi ya pamoja yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha mapokezi ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kufanya ziara yaikikazi ya siku saba mkoani humo Februari 23.

Matembezi hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Burian na yalibeba kauli mbinu ‘Amka na Samia.’

Akizungumza mara baada ya matembezi hayo, Dk Burian amewataka wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Samia.

“Ni heshima kubwa kwa Mkoa wa Tanga kumpokea Mheshimiwa Rais. Tunapaswa kuonyesha mshikamano wetu kwa kujitokeza kwa wingi siku ya mapokezi yake, ambayo ni kesho Serikali yake imefanya kazi kubwa ya maendeleo, na ni fursa yetu kuthibitisha uungwaji mkono wetu kwake,” amesema Dk Burian.

Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo wamesema uongozi wa Rais Samia umeleta maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali, zikiwemo miundombinu, elimu, afya na biashara.

Akiwa mkoani Tanga Rais Samia anatarajiwa kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Related Articles

Back to top button