Ligi KuuNyumbani

Mashabiki 4 Namungo wafariki dunia

WATU wanne wamekufa na wengine 16 kujeruhiwa baada ya gari lililokuwa likiwasafirisha mashabiki wa klabu ya Namungo kwenda Dar es Salaam kupata ajali eneo la Miteja karibu na Somanga mkoani Lindi.

Taarifa ya klabu ya Namungo imesema majeruhiwa wamepelekwa katika kituo cha afya Tingi wilaya Kilwa mkoani Lindi.

“Uongozi wa Klabu ya Namungo FC umepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya mashabiki wetu waliokuwa wakisafiri kutoka Ruangwa kuelekea Dar es Salaam kuishangilia timu yao kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga sc mchezo utakaofanyika leo tarehe 20 Septemba 2023,”imesema taarifa hiyo.

Nayo timu ya Yanga imetuma salamu za pole kwa klabu ya Namungo kufuatia tukio hilo.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa uongozi wa Namungo fc na familia zote kufuatia vifo vya mashabiki wanne waliofariki kwenye ajali ya gari iliyokuwa ikiwaleta Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi yetu utakaofanyika leo katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi,”imesema klabu ya Yanga.

Mchezo huo kati ya Yanga na Namungo ni mechi pekee ya Ligi Kuu leo.

Related Articles

Back to top button