Mastaa

Rayvan, Vera Sidika waweka wazi kilichokwamisha shoo ya Toronto

TORONTO: MWANAMUZIKI Rayvanny anayetokea Tanzania na mwenzake Vera Sidika anayetokea Kenya wameweka wazi kilichowakwamisha hadi wakashindwa kufanya onyesho lao katika jiji la Toronto nchini Canada.

Rayvan akisapotiwa na Vera Sidika katika ukurasa wake wa Instagram alionyesha kusikitishwa kwake huku akidai kuwa vurugu alizozikuta ukumbini ncizo zilizochangia kushindwa kufanya onyesho lao katika ukumbi huo.

“Nawasikitikia sana mashabiki wangu wa Toronto. Nilijiandaa na kujipanga kwa ajili ya shoo, lakini yaliibuka masuala mengi ambayo yalizuia kutokea. Nilichelewa sana kufika na wakati nilipofika ukumbini kulikuwa na kutoelewana. Nilisafiri kwa saa nyingi kukuburudisha, lakini kwa bahati mbaya, sikuweza kujiunga nawe leo. Najua umekata tamaa sana, na samahani sana.,” aliandika Rayvan.

Hata hivyo Rayvan ameahidi kwamba atakaa na waandaaji wa onyesho hilo na watatangaza tarehe mpya ambapo kila aliyenunua tiketi ataingia bure.
Vera aliunga mkono maoni ya Rayvanny, akishiriki ujumbe wake na kueleza kwamba fujo ilitokea.

“Baada ya safari ndefu ya ndege na kuwa tayari kwa wakati hata sikupumzika, nyote mnajua kosa halikuwa letu ilikuwa nje ya uwezo wangu,” aliandika Vera.

Vera pia alitarajiwa kuhudhuria Tamasha la Kiswahili lakini alishindwa kufika kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Related Articles

Back to top button