FANyumbani

Raundi ya awali FA Nov 5, 6

MICHEZO ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA itafanyika Novemba 5 na 6.

Kwa mujibu wa ratiba Kigoma Kwanza ya Kigoma itavaana na Kakubilo ya Geita katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma Novemba 5.

Katika mchezo mwingine Buhare ya Mara itakuwa mgeni wa Lamadi ya Simiyu katika uwanja wa Halmashauri, Simiyu.

Novemba 6 Kibadeni ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Tandika United ya Dar es Salaam kwenye uwanja wa shule ya Minaki mkoani Pwani.

Nayo Kawele ya Kilimnjaro itakuwa mgeni wa Misitu ya Tanga katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button