Nyumbani

Dabo kutuma makachero APR

ZANZIBAR: KOCHA Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema licha ya kuendelea na maandalizi ya msimu mpya, wanatafuta taarifa za mpinzani wao APR FC, watakaekutana nae katika mchezo wa hatua za awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dabo amesema mechi yao na APR FC itakuwa ya kawaida kama ilivyo kwa michezo mingine lakini hawataichukulia poa kwa sababu katika mashindano hayo kila timu inafanya maandalizi mazuri ya kusonga mbele.

Azam FC wapo visiwani Zanzibar na baadae wanatarajia kwenda nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 yaliyopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Msimu uliopita hatukufanya vizuri katika michuano hii na kushindwa kuingia makundi, safari hii tunajipanga vizuri. Naanda timu imara wachezaji wapya na waliopo msimu uliopita kuungana” amesema kocha huyo.

Dabo ameongeza kuwa walijiandaa kukutana na timu yoyote kwenye hatua hiyo na anamatarjio makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya APR FC na kuingia hatua ya makundi.

Dabo amesema licha ya kufanya maandalizi mazuri lakini pia wanahitaji kuwafatilia wapinzani wao hao wanavyocheza wanapokuwa nyumbani na ugenini, wataingia kwa tahadhari kubwa kwa sababu ya ubora wa wapinzania wao hao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button