Funguo imechagua milango ya NBCPL
DAR ES SALAAM: KIUNGO na kinara wa mabao wa Yanga, Stephane Aziz Ki amekata mzizi wa fitna na kuamua kuchagua kubaki kwa waajiriwa wake hao kwa msimu wa 2024/25.
Taarifa zinasema kuwa kiungo huyo ameamua kuendelea na Yanga kwa sababu kuna mambo mengi wamekubaliana na Rais wa timu hiyo, Eng Hersi Said.
Aziz Ki ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kutumikia klabu hiyo baada ya wa hapo awali kufikia tamati mwisho mwa msimu uliopita huku akiachana na ofa nyingi zilizkuweopo mezani zikiwemo Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs za Afrika kusini.
Pia inadaiwa kuwa CR Belouizdad ya Algeria, iliweka ofa ya mshahara wa Sh milioni 97, jumla ya Milioni 291 kwa miezi mitatu pamoja na nyumba, gari na tiketi mbili za ndege yenye hadhi ya juu.
“Nimerejea nchini kujiunga na wachezaji wenzangu kwa ajili ya kusaidia kwa msimu mpya wa mashindano na malengo ni kuona Yanga inacheza fainali za Afrika,” amesema kiungo huyo.
Kiungo huyo ameingia kambini leo Avic Town, Kigamboni kuungana na wachezaji wenzake kujiangaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.