Ramovic: Vilio sasa basi
RUANGWA: KUELEKEA mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Namungo FC, Kocha Mkuu wa wa Yanga, Saed Ramovic amedai kuwa wanatakiwa kulipa deni la mashabiki wa timu hiyo kuwarejeshea furaha iliyopotea.
Amesema wana mchezo mgumu na muhimu kesho ,maandalizi yameenda vizuri kila kitu kipo vizuri wanafahamu Namungo wana wachezaji wazoefu lakini watapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwa ajili ya mashabiki wa Yanga na heshima ya klabu hiyo.
“Hatupo hapa kutafuta kingine zaidi ya alama tatu, kwa kweli ni jambo la kujivunia sana, mimi na wachezaji wangu tunapaswa kuwalipa furaha mashabiki wetu,” amesema.
Ramovic amesema mashabiki wameonesha moyo na mapenzi ya dhati kwa timu kwa kusafiri kila timu inapokwenda na kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kupambana kutafuta alama tatu dhidi ya Namungo FC.
Yanga imepoteza michezo mitatu mfulululizo iliyocheza jambo lililowavunja moyo baadhi ya mashabiki wa timu hiyo lakini kocha Ramovic amewaahidi furaha mashabiki hao kwa mara nyingine.