Wimbo ni Yanga ashinde au Mazembe afungwe

DAR ES SALAAM:MUDAmfupi ujao wawakilishi wa pekee wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika Young Africans Sports Club watakuwa na kibarua kizito cha kuiheshimisha nchi mbele ya kunguru wa Lubumbashi TP Mazembe majira ya saa 10 jioni.
Mchezo huu ni wa Nne kwa Yanga katika hatua hii ya makundi na watakuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza baada ya kuambulia sare moja katika michezo mitatu iliyopita na kupoteza miwili dhidi Al Hilal na MC Alger.
Hata hivyo, mashabiki wa Yanga wameonekana kuwa na imani kubwa na timu hiyo huku wengi wakielekea dimba la Benjamin Mkapa kuishangilia klabu yao pendwa wakiwa na imani kwamba leo kwa namna yoyote ile Yanga lazima ashinde na kama si hivyo basi TP Mazembe lazima afungwe.
Umeelewa au tuwaachie wenye D mbili?
Kila la kheri Yanga!