Ligi Daraja La Kwanza

Polisi yaita mashabiki ikivaa Kiluvya kesho

KILIMANJARO: TIMU ya Polisi Tanzania imeita mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono kuelekea mchezo wa Ligi ya Championship dhidi ya Kiluvya United utakaochezwa katika Uwanja wa Ushirika Moshi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa habari wa timu ya Polisi Tanzania Inspekta Frank Lukwaro, kikosi hicho kinaendelea na mazoezi ili kuhakikisha kuwa kinapata alama tatu katika uwanja wake wa nyumbani.

“Ili timu ipate matokeo mazuri inahitaji mashabiki wengi wajitokeze kwa wingi kutoa hamasa kwa wachezaji wapate morali ya kupambana uwanjani, tunawahimiza mashabiki zetu waje kwa wingi,”alisema.
Mpaka sasa timu ya Polisi ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama 20 baada ya kucheza michezo 17.

Related Articles

Back to top button