Pep atema nyongo, ni kiburi haswa!
LONDON, ENGLAND :Meneja wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester city Pep Guardiola amesema hatatumia kikosi chake cha kwanza katika michuano ya Kombe la Ligi maarufu Carabao Cup.
Akizungumza baada ya mchezo wa kikosi chake dhidi ya Watford Pep amesema katika raundi ijayo ya mashindano hayo hatatumia wachezaji wake wa kikosi cha kwanza badala yake atatumia wachezaji ambao hawapati nafasi au wale wa kikosi cha pili.
“Nasema hapa raundi ijayo tutatumia wachezaji wanaocheza dakika chache au wa kikosi cha pili, Hatutapoteza nguvu zetu kwa michuano kama hii, sijui itatokea nini lakini kama tutaendelea kuwa na majeraha kwenye timu” amesema
Guardiola pia amesema haidharau michuano hiyo na ni michuano mizuri na yenye msisimko lakini anataka kuwekeza zaidi nguvu zake kwenye michuano yenye msisimko zaidi
Katika mchezo wao wa raundi ya 3 ya Kombe la Carabao wababe hao wa England waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mabao ya Jeremy Doku na Matheus Nunes kabla ya Watford kujibu dakika za jioni kwa bao la Thomas Ince dakika ya 86.