Muziki

Pablo ataja sababu za Nyashinski kuondolewa kwenye ‘Mvua ya Baraka’

DAR ES SALAAM: MTAYARISHAJI wa muziki, Pablo, amefafanua sababu za msanii wa Kenya, Nyashinski, kuondolewa kwenye wimbo Zuchu ‘Mvua ya Baraka’.

Pablo amesema uamuzi wa kuondoa Nyashinski katika wimbo huo ulitokana na msanii huyo kuwa na ratiba nyingi na kushindwa kupatikana wakati ambao kazi hiyo ilihitaji kukamilishwa kwa haraka.

Akieleza sababu hizo, Pablo amesema “Nyashinski alikuwa amesafiri wakati ambapo Zuchu anahitaji kufanya maandalizi ya mwisho ya wimbo huo, ikiwemo kurekodi video yake ili kazi hiyo itoke kwa wakati uliopangwa.

Amesema “hali hiyo ilimfanya Zuchu kushindwa kuendelea na mpango wa awali wa kumshirikisha msanii huyo, huku kukiwa na uamuzi kwamba haikuwa sahihi kutoa audio pekee bila kukamilisha mpango wa kuitangaza kazi hiyo kwa picha.

Kutokana na mazingira hayo, “Zuchu aliamua kuendelea na mpango wa kutoa wimbo huo bila ushiriki wa Nyashinski badala ya kuchelewesha uzinduzi wake kwa sababu ya kutokuwepo kwa msanii huyo.

Hatua hiyo imeweka wazi kuwa kuondolewa kwa Nyashinski hakukutokana na sababu za kisanii au kutokuelewana, bali changamoto ya ratiba na muda wa kukamilisha mradi huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button