Muziki

One Direction, Simon Cowel wamuaga Liam Kanisani

LONDON : NYOTA wa muziki wanaounda kundi la One Direction, Harry Styles, Niall Horan, Zayn Malik na Louis Tomlinson ni miongoni mwa maelfu ya wahudhuriaji katika misa ya kumuaga mwanamuziki mwenzao Liam Payne aliyefariki jijini Buenos Aires nchini Argentina baada ya kudondoka kutoka ghorofa ya tatu ya hotelini Oktoba 16mwaka huu

Wanamuziki hao walikuwa miongoni mwa waombolezaji katika ibada ya mazishi ya Liam katika Kanisa la St Mary’s huko Amersham, kusini-mashariki mwa Uingereza.

Cheryl, mpenzi wa zamani wa Liam na mama wa mtoto wake wa kiume Bear mwenye umri wa miaka saba, amehudhuria ibada hiyo pamoja na wenzake wa Girls Aloud Nicola Roberts na Kimberley Walsh.

Cheryl mwenye miaka 41, amekuwa kwenye uhusiano na Liam kati ya 2016 na 2018, na kufuatia kifo chake, ameelezea katika taarifa yake kwamba alimpenda sana nyota huyo wa pop.

Kate Cassidy, mshawishi wa mitandao ya kijamii ambaye alikuwa na Liam kabla ya kifo chake walikuwa na uhusiano kuanzia Oktoba 2022 hadi kifo chake, naye alifika kanisani na mtoto wa mwigizaji Elizabeth Hurley, Damian Hurley kwa ajili ya misa ya kumuaga mwanamuziki huyo.

Naye mwendesha kipindi cha American Got Talent, Simon Cowell alihudhuria ibada hiyo pamoja na mshirika wake Lauren Silverman.

Simon Cowel mwenye miaka 65 alichukua jukumu la kufanyakazi na na Liam, Pamoja na kuendeleza kundi la One Direction baada ya kuingiza katika shindano la ‘The X Factor’ mwaka wa 2010.

Related Articles

Back to top button