Muziki

Zabron Singers yapata pigo

DAR ES SALAAM :MSANII wa Kundi la Muziki la Zabron Singers, Marco Joseph amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 22 katika Taasisi ya Moyo wa Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha msanii huyo zimethibitishwa na Japhet Zabron ambaye ni msanii mwenzake wakati akifanya mazungumzo na SpotiLeo.
” Nikweli Marco Joseph amefariki, ni gafla tu mshtuko wa moyo alianza kuugua Jumapili iliyopita ukiachana na Jumapili hii, alikuwa hasumbuliwi na maradhi yoyote kabla” amesema Zabron.
Enzi za uhai wake Joseph alishiriki katika nyimbo mbalimbali za dini ndani ya kundi hilo zilizokonga watu kwa namna tofauti huku kumbukumbu za wimbo wa ‘Upo Single’ zikiwa kivutio kikubwa katika kazi yake.

Related Articles

Back to top button