Odemba awachana walimbwende wa kisasa

DAR ES SALAAM : MLIMBWENDE wa zamani wa Tanzania, Miriam Odemba, ameibua mjadala mitandaoni baada ya kuwakosoa walimbwende wa kizazi cha sasa kwa madai kuwa wamepoteza uhalisia na mvuto wa asili uliokuwepo zamani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Odemba amesema walimbwende wa sasa wamejikita zaidi kwenye muonekano wa kisasa usio wa asili badala ya kuonesha urembo wa Kiafrika.
“Mnichukie au mnipende, lakini hii ni wazi kabisa kwa walimbwende wa Tanzania.
Kwa kweli siku hizi hakuna kabisa walimbwende kama wa zamani enzi zetu. Sasa hivi wengi wamekuwa kama ‘masanamu’, ule uhalisia na uafrika wa asili unapotea,” ameandika Odemba.
Aidha, Odemba amehoji matumizi makubwa ya makeup, wigs pamoja na muonekano wa kisasa unaodaiwa kufunika uhalisia wa washiriki wa mashindano ya urembo.
“Halafu mnajiona nyie ndio kila kitu, mikope, migundi … waandaaji wa mashindano mnashindwa nini kutoa walimbwende wa asili natural?” ameongeza.




