Tetesi

Partey kipaumbele mbadala wa Pogba

HOFU iliyotokana na tukio la Paul Pogba kugundulika kutumia dawa ya kusisimua misuli imesababisha mkurugenzi wa michezo wa Juventus ‘Bianconeri’, Cristiano Giuntoli kutafuta viungo kuziba pengo.

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo Calciomercato wa Italia, miamba hiyo ya Serie A imeorodhesha wachezaji kadhaa inaoona wanafaa kuchukua nafasi hiyo.

Kiungo wa ‘Washika mtutu’ wa London, Arsenal, Thomas Partey anapewa nafasi ya kwanza katika orodha hiyo, huku Washika mtutu hao wakiripotiwa kuwa tayari kumruhusu Partey mwenye umri wa miaka 30 kuondoka Emirates.

Khephren Thuram wa Nice ni mchezaji Giuntoli anaona kivutio, lakini pia anaweza kuwa ghalia zaidi kwenye orodha hiyo mwenye thamani ya Euro milioni 35 sawa na shilingi bilioni 91.94.

Juve pia inasaka saini ya Manu Kone wa Borussia Monchengladbach, ambaye awali aliwaniwa na AC Milan wakati akikiwasha Toulouse ya Ufaransa na amekuwa katika kiwango bora tangu alipohamia Bundesliga.

Kiungo wa Strasbourg, Habib Diarra ndiye anayefuata katika orodha lakini Juve inaweza kukabiliwa na ushindani mkubwa kutoka Wolfsburg katika kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 anayekadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni 20.

Mchezaji wa mwisho katika orodha hiyo ni Abdoulaye Kamara kutoka Borussia Dortmund, ingawa Bianconeri itakuwa inamsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 kama tegemeo la baadaye kuliko wa kikosi cha kwanza kwa sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button