Tetesi

Man United yawania saini ya Olmo

TETESI za usajili zinasema Manchester United imeingia katika mbio za kumsajili winga wa kimataifa wa Hispania Dani Olmo, ambaye ana kipengele cha kuachiwa toka RB Leipzig cha pauni milioni 52 majira yajayo ya kiangazi.

Winga huyo mwenye umri w miaka 25 pia anawaniwa na Real Madrid, Manchester City, Chelsea na Tottenham. (Mail)

Barcelona inaweza kumkosa kiungo wa Kijerumani Joshua Kimmich, 29, kutokana na Manchester United kuwa tayari kumsajili nyota huyo wa Bayern Munich majira yajayo ya kiangazi. (Sport – in Spanish)

Manchester City na Newcastle United zitashindana na Manchester United kumsajili beki wa kati wa Everton na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Jarrad Branthwaite, 21. (Football Transfers)

Liverpool, Borussia Dortmund na RB Leipzig zipo tayari kumgombea Dean Huijsen, 18, wa Juventus huku beki huyo wa kihispania akionesha kiwango msimu huu akiwa kwa mkopo katika klabu ya Roma. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Crystal Palace inataka kumsajili beki wa Valencia, Cristhian Mosquera, 19, majira yajayo ya kiangazi lakini inakabiliwa na ushindani toka Atletico Madrid. (Evening Standard)

Related Articles

Back to top button