EPL

Nuno na moto wake Nott’m Forest

LONDON: Meneja wa Nottingham Forest Nuno Espirito Santo amesema hajashangazwa na mwanzo mzuri wa klabu yake katika msimu wa huu wa Ligi Kuu Engand licha ya kumaliza juu kidogo ya mstari wa kushushwa daraja msimu uliopita.

Forest, ambao walimaliza katika nafasi ya 17 kati ya timu 20 za ligi msimu uliopita, wapo nafasi ya 5 kwenye msimamo wakiwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo 11 watasafiri hadi London kuwafuata Arsenal walio nafasi ya nne.

Nottingham Forest hawajapoteza ugenini msimu huu, na mchezo huu dhidi ya Arsenal utatazamwa na wengi kama kipimo sahihi cha uwezo wa kocha Nuno kwenye michezo mikubwa baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea November 10 mwaka huu.

“Ninachotarajia ni wachezaji wetu kujituma kwa hali ya juu kabisa kufanya mambo sawa. Kwa nje inaweza kuwa ya kushangaza lakini kwetu? Hapana. Tunafanya nao kazi kila siku, tunajua ubora na vipaji walivyonavyo, tunataraji mengi kutoka kwao lakini tunapaswa kuwa wavimilivu na kutambua ni msimu bado mrefu na mgumu sana.” alisema

Forest waliwaduwaza vinara Liverpool 1-0 katika uwanja wa Anfield mwezi Septemba na huenda wakafanya maajabu mengine dhidi ya Arsenal hapo kesho dimbani Emirates.

“Tutakutana na timu nzuri na ngumu. Tutapambana kufanya kila kitu, lakini utakuwa mchezo mgumu,” meneja huyo Mreno aliongeza.

Related Articles

Back to top button