Nottingham forest yasaka ‘Digital manager’ mpya
NOTTINGHAM: Siku chache baada ya klabu ya Nottingham forest kupigwa faini ya pauni Laki 720 baada ya chapisho lake kwenye mtandao wa X wa klabu hiyo kumkashifu mwamuzi wa VAR Stuart Attwell klabu hiyo imetangaza kumtafuta meneja mpya wa mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa X Nottingham forest walichapisha chapisho lililotafsiriwa na kamati ya Waamuzi wa Premier League PGMOL kama shambulio kwenye uadilifu wa muamuzi huyo raia wa England baada ya mchezo wao dhidi ya Everton wa Aprili 21 mwaka huu.
Katika mchezo huo waliopoteza kwa mabao 2-0 Forest waliamini walistahili kupewa penalti 3 ambazo zilikataliwa baada ya kuwekwa chini ya mapitio ya VAR iliyokuwa ikisimamiwa siku hiyo na Attwell.
Baada ya mchezo huo katika ukurasa wa X wa Nottingham Forest lilionekana chapisho lililodai kuwa muamuzi huyo ni shabiki wa Luton Town suala lililoikasirisha bodi hiyo ya waamuzi iliyosema ni shambulio dhidi ya uadilifu wa mwamuzi huyo
‘Tuliionya bodi ya PGMOL kwamba mwamuzi wa VAR ni shabiki wa Luton kabla ya mchezo lakini hawakumbadilisha. Uvumilivu wetu umejaribiwa mara nyingi. NFFC sasa itaangalia hatua nyingine.’ lilisomeka chapisho hilo
Kutafutwa huko kwa meneja mpya wa mitandao ya kijamii kunatafsiriwa kama hatua ya uongozi wa klabu hiyo kujitenga na kile ambacho wadau wengi wa soka nchini England wamekiita kama kuvuja kwa kitengo hicho.