AfricaAfrika Mashariki

Tanzania bingwa CECAFA U18 wanawake

TANZANIA leo imetwaa ubingwa wa michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 baada ya kuikanda Uganda kwa bao 1-0 katika mchezo wa mwisho.

Bao pekee la ushindi la Tanzania katika mchezo uliofanyika uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam limefungwa na Winifrida Gerald katika dakika ya 42 kwa kiki kali baada ya kukutana na mpira uliogonga mwamba na kurejea uwanjani.

Uganda ambayo ilikuwa na pointi 9 sawa na Tanzania kabla ya mchezo wa leo imeshika nafasi ya pili huku timu nyingine zilizoshiriki michuano zikiwa ni Burundi, Ethiopia na Zanzibar.

 

Related Articles

Back to top button