EPL

Ni Ndoto, matumaini Potter akitua West Ham

LONDON: West Ham united wamemtangaza rasmi meneja wa zamani wa Chelsea Graham Potter kuwa mkufunzi mkuu wa kikosi hicho chenye maskani jijini London akichukua nafasi ya Julen Lopetegui ambaye amefungashiwa virago.

Graham Potter mwenye miaka 49 anarudi kwenye kazi za ukocha baada ya kuwa nje ya kazi hiyo tangu alipoachana na Chelsea Aprili mwaka 2023 na amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu akibeba matumaini ya klabu hiyo kujinasua kutoka nafasi ya 14 point saba pekee kutoka eneo la kushuka daraja.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imemnukuu kocha huyo akijinasibu kufanya vizuri huku akisema kazi hiyo ni sahihi na imekuja wakati sahihi kwake

“Ni muhimu nimekaa mda mrefu mpaka kupata kazi hii, nahisi ni wakati sahihi kwangu na mimi ni mtu sahihi kwa kazi hii. Mazungumzo yangu na mwenyekiti wa klabu yamekuwa na faida, tupo safari moja ya kujenga msingi imara kwa ajili ya kusonga mbele” – amenukuliwa

Related Articles

Back to top button