Neymar atemwa kikosi cha Brazil

BRASILIA, Brazil
MCHEZAJI wa timu ya taifa ya soka ya Brazil, Neymar Junior, ametemwa kwa mara nyingine kwenye kikosi kilichotangazwa na kocha mkuu Carlo Ancelotti kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa za kalenda ya FIFA kuelekea maandalizi ya FIFA World Cup 2026.
Brazil inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki, ikianza kwa kuchuana na Ufaransa katika mchezo utakaopigwa Machi 26, 2026 mjini Boston, Massachusetts, Marekani, kabla ya kuikaribisha Croatia kwenye mchezo mwingine utakaochezwa mjini Orlando, Florida.
Katika kikosi hicho, mshambuliaji kinda Endrick amerudi tena baada ya kuonesha kiwango bora ndani ya miezi mitatu akiwa na klabu ya Olympique Lyonnais.
Akizungumza baada ya kutangaza kikosi hicho, Ancelotti amesema Neymar bado ana nafasi ya kurejea kwenye timu hiyo kuelekea Kombe la Dunia, lakini anatakiwa kwanza kurejea kwenye kiwango chake cha juu.
Kocha huyo ameongeza kuwa hajaamua kumuita mshambuliaji huyo kwa sasa kwa sababu bado hajafikia kiwango kinachotakiwa, akisisitiza kuwa timu inahitaji wachezaji walio kwenye ubora wao ili kuisaidia Brazil kufanya vizuri kimataifa.




