Kwingineko

Kisa ‘anthem’ UEFA, Aston villa wajieleza

BIRMINGHAM:KLABU ya Aston villa na Shirikisho la Soka bara Ulaya UEFA wamelazimika kutolea maelezo tukio la kuchezwa ‘anthem’ tofauti na ile ya UEFA Champions League kabla ya kuanza kwa mchezo wa mkondo wa pili wa ligi hiyo kati ya Aston villa na PSG usiku wa kuamkia leo.

Katika hali isiyo ya kawaida spika za uwanja wa Villa Park zilipeperusha wimbo wa Europa League badala ya ule wa UEFA Champions League kwa sekunde kadhaa wakati vikosi vya timu hizo vikiingia uwanjani kwa ajili ya kipute hicho kuanza kabla ya wimbo huo kubadilishwa na kupigwa ule wa UEFA Champions League.

Vyanzo vya ndani ya klabu na shirikisho la UEFA vimeiambia BBC sport kuwa tatizo la kiufundi katika mfumo wa sauti wa uwanja huo ambao ni mfumo wa kujiendesha yaani Automatic ulipata hitilafu ya kuingiliwa na mfumo mwingine kisha kusababisha wimbo huo kuchezwa kitendo ambacho kiliwaacha wachezaji na mashabiki midomo wazi.

Beki wa Aston Villa Ezri Konsa aliweka kiganja cha mkono wake kwenye paji la uso wake wakati yeye na mchezaji mwenzie kiungo Youri Tielemans wakijaribu kuzuia kicheko, huku Fabian Ruiz wa PSG na Ousmane Dembele wakitazamana kwa mshangao.

Hata hivyo Aston Villa hawatakumbana na adhabu yeyote kwakuwa hakuna kanuni inayozungumzia suala la kupigwa nyimbo tofauti katika kanuni zinazoongoza michuano hiyo pendwa zaidi Ulimwenguni.

Related Articles

Back to top button