World Cup
New Zealand yaanza kwa moto Kombe la Dunia wanawake
NEW Zealand imeanza vema fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake 2023 baada ya kuifunga Norway kwa goli 1-0 katika mchezo wa ufunguzi wa kundi A.
Goli hilo limefungwa na Hannah Wilkinson katika dakika ya 43 huku Ria Percival akiinyima New Zealand goli lingine baada ya kukosa penalti dakika 90 wakati wa mchezo huo uliopigwa uwanja wa Eden Park, jijini Auckland.
Mataifa ya Afrika yataanza kampeni Julai 21 kwa Nigeria kupambana na Canada ambapo nchi nyingine za bara hilo zinazoshiriki fainali hizo ni Zambia, Afrika Kusini na Morocco.




