Muziki
Mzee Yusuph: “Nikisoma mashairi yangu, hata mimi nashangaa nilivyoandika”

DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Taarab, Mzee Yusuph, amesema kwa sasa maisha yake yamebadilika na hafuati tena mambo aliyokuwa akiyapitia zamani.
Akizungumza na Spoti leo kwa hisia, amesema kuwa kila anaposoma mashairi aliyowahi kuyaandika, hujikuta akijiuliza kama kweli ni yeye aliyeyaandika kutokana na uzito wa ujumbe uliomo.
“Nikila ninapepewa na mwili na suguliwa, lakini sasa hivi nalabwa, sisuguliwi tena. Yaani nilivyoandika mashairi haya hadi sasa najiuliza, kweli ni mimi niliandika?” amesema.
Mzee Yusuph ameongeza kuwa kwa sasa hasubiri mtu mwingine amletee furaha, bali anajitengenezea mwenyewe.
“Raha singoji kupewa, naajipa mwenyewe. Jamani, naona nitachelewa kidume kula maini,” amemaliza kwa utani.




