Muziki

Lady Gaga kuachia albamu ya ‘Joker’ Ijumaa

NEW YORK: Nyota wa muziki wa pop, Lady Gaga ametangaza mipango ya kutoa albamu yake mpya yenye nyimbo 13, iitwayo ‘Harlequin’.

Mwanamuziki huyo mwenye miaka 38 amesema albamu yake hiyo ataiachia siku ya Ijumaa Agosti 27 mwaka huu wa 2024.

Nyota huyo aliyeonekana pamoja na Joaquin Phoenix katika filamu mpya ya kusisimua ya kisaikolojia, ambaye anacheza Harley Quinn katika mwendelezo wa ‘Joker’ ya 2019 ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Harlequin. Septemba 27. Albamu mshirika wa Joker: Folie a Deux. (sic)”

Kwa siku kadhaa Lady Gaga amekuwa akitania mara kwadhaa kuhusu albamu hiyo mpya kwenye mitandao ya kijamii akichapisha jumbe za mafumbo kama, “Niko tayari kwa mahojiano yangu” na “Usiniambie nivae nini”.

Orodha ya nyimbo za albamu hiyo mpya ni inapendekeza kwamba kava za ‘Joker: Folie a Deux’, kama vile ‘Oh, When the Saints’, zitachanganywa na nyingine mpya.

Akiongea na Vogue, Lady Gaga alisema: “Nilikuwa na mpiga kinanda, Alex Smith, ambaye nilimwomba awe pamoja nami kwa matukio yangu. Kuna nyakati katika filamu ambapo ninacheza mwanamke mtu mzima ambaye anaimba kama msichana mdogo nilikuwa naye na nasonga naye kote ulimwenguni kwa sababu inapendeza,”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button