Filamu 65 zatangazwa kuwania tuzo za ZIFF 2026o

ZANZIBAR:TAMASHA Kimataifa la filamu Afrika Mashariki, Zanzibar International Film Festival (ZIFF), limeanza kuteka headlines baada ya waandaaji wake kutangaza rasmi filamu 65 pekee kutoka nchi mbalimbali duniani ndizo zitakazosshindanishwa katika tamasha hilo.
Nchi ya Uganda imeongoza kwa kuwasilisha filamu 50 katika tamasha hilo huku Tanzania ikiwasilisha filamu 45 tu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tamasha hilo Joseph Mwale amesema licha ya kupokea filamu nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani lakini filamu hizo tu ndizo zitapata nafasi ya kuoneshwa kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa.
Mwale amesema Katika Tamasha hilo mwaka huu mada kubwa ni matumizi ya Akili Mnembe (AI) kwenye uandishi wa Hadithi na uandaaji wa filamu.
Tamasha hilo ambalo ni miongoni mwa matukio makubwa zaidi ya sanaa na filamu barani Afrika, linatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar kuanzia Juni 21 hadi 24, 2026 huku likitarajiwa kuwakutanisha watengeneza filamu kutoka nchi mbalimbali, waigizaji, waandaaji wa filamu na watengeneza maudhui mtandaoni pamoja na wadau wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali duniani.




