Nyumbani

Mwasyoge: Michezo ni nguzo ya kuimarisha amani

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), David Mwasyoge, amesema michezo ina nafasi kubwa katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Mwasyoge ameyasema hayo wakati akizungumza na Dailynews Digital kuhusu nafasi ya michezo katika amani ambapo amesema kuwa michezo hujenga mshikamano wa kijamii bila kujali tofauti za kidini, kisiasa au kikabila.

“Watu kutoka maeneo tofauti tumekutana kama familia moja. Kilichotuleta pamoja ni michezo ya kuogelea, na tunafanya kazi kwa pamoja. Umoja huu wa timu kwenye mchezo huu unanipa faraja kubwa,” amesema Mwasyoge.

Amesema kuwa umoja na mshikamano unaopatikana kupitia michezo unapaswa kuwa mfano kwa Watanzania wote, akihimiza jamii kujihusisha zaidi na michezo kama njia ya kudumisha amani na kuelewana.

“Michezo inawakutanisha watu wa aina mbalimbali, dini tofauti na itikadi tofauti, lakini wote wanakuwa na lengo moja. Hii ni njia nzuri ya kuimarisha amani na mshikamano katika jamii,” ameongeza.

Mwisho

Related Articles

Back to top button