Kwingineko

Mutale, Che Malone kukipiga Stars?

DAR ES SALAAM:  UONGOZI wa klabu ya Simba umeandika barau na kuipeleka kwa Kamishna Jenerali Uhamiaji kuwaombea uraia wa Tanzania kwa wachezaji wao wa kigeni.

Barua iliyoandikwa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu imeeleza kuwa Simba inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa kwa mujibu wa kanuni za usajili za TFF, Klabu ya ligi kuu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni 12 katika msimu mmoja wa ligi.

Imesema kuwa Simba ina wachezaji wa kigeni ambao wamekua na mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu kimpira na kutoa uwakilishi mzuri kimataifa.

“Wachezaji hao wamekua wakikosa nafasi katika nchi zao hususan timu za taifa, kwa kuzingatia mahitaji ya klabu na mchango wa wachezaji hao, Simba inaomba wachezaji tisa (9) wa kigeni waweze kupatiwa uraia wa Tanzania, ili waweze kufanya kazi kama watanzania,”.

Miongoni mwa wachezaji wa kigeni ambao hawana nafasi ya kucheza katika Mataifa yao ni winga Joshua Mutale na beki Che Malone Fondoh

Barua hiyo imeeleza sababu ya maombi haya ni kwamba wachezaji hao bado ni vijana wana muda mrefu wa kutumika Tanzania.zaidi, wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.

“Tunaomba pia wakati wa mchakato huu, wachezaji hao ambao orodha yao imeambatanishwa wahesabike kama Watanzania na kuondoshewa malipo yote yanayotakiwa kufanywa kwa mchezaji wa kigeni.

Kwa barua hii, tunaomba ofisi yako iridhie maombi yetu na kutupa taratibu husika ili kukamilisha mchakato, imani yetu kuwa ombi hili litashughulikiwa ipasavyo kutokana na maamuzi ya Serikali kuruhusu mchakato wa aina hiyo kufanyika.

Alipotafuta Meneja wa idara ya Habari na mawasiliano ya klabu hiyo, Ahmed Ally amesema hiyo barua imeandikwa na mwenyekiti wa klabu hiyo hana cha kitu kuongezea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button