Muna Love aachia ujumbe mzito baada ya kujifungua

Msanii wa filamu nchini, Rose Alphonce ‘Munalove’ amejifungua mtoto mwingine wa kiume baada ya kupitia maumivu na kejeli nyingi kufuatia kumpoteza mtoto wake Patrick, ambaye alifariki Julai 3,2018.
Muna Love ameweka picha akiwa na mtoto wake mchanga wakiwa Hospitali nchini Canada na kuacha andiko lililowagusa wengi huku akiomba ulinzi kwa mtoto wake na kumkabidhi mikononi mwa Yesu.
Pia, anawaombea wale wenye uhitaji na waliokata tamaa, wakijazwa imani kama yeye alivyojazwa.
Mwisho, anamtaja Patrick na kumshukuru Yesu kwa kumpa mtoto wa kiume tena, ambaye anaitwa “Testimony” na jina lingine la Kiislamu ambalo atalitaja baadae.
Muna ameandika “Asante Yesu kwanirudishia zaidi ya kile ulichochukua, nikisema nianze kuelezea Matendo yako Makuu juu yangu sitamaliza. Walinipiga fimbo nyingi za maumivu 9maneno ya kejeli na kila walichoona nastahili.
“Lakini sikuchoka Neno langu lilikua wakati nalia kwa uchungu ndani ikiwa mbele zao najikaza najifanya siumii nilikua nakuambia kwa uchungu wewe Yesu unajua ukweli unanijua niponye wewe Yesu unaona naomba tu niponye uchungu huu haya maneno leo najivunia. Yesu Asante
“Nilikuahidi kua ukinipa mtoto yoyote tena nikakuomba arudi tu kama yulee atafanya kazi yako kwa Dini zote na nitakutangaza kama chizi nitasimulia Matendo yako Makuu bila aibu nitajivunia wewe popote na hata sasa umejibu makubaliano yetu.”
“Yesu kama ulivyonipa nakuomba unajua kukutangaza wewe ni vita namfunika mwanangu kwa Damu yako Takatifu atakemgusa au kumnenea mabaya akakutane na wewe.
“Mimi siwezi siwezi zuia chochote Baba yangu ile ahadi niliyo kuahidi Ntafanya apa apa walikonikejeli na kunichapa fimbo za maneno nitawaonyesha Ukuu wako najua unaona Yesu ila ulinzi wako Baba kwakua sehemu ni hii Yesu Namkabidho mwanangu Testmony mikononi mwako, ameandika msanii huyo.