Filamu

Filamu ya Kenya kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu

NAIROBI: FILAMU ya kusisimua ya ‘2 ASUNDER’ yenye dakika 85 iliyoandaliwa katika Jiji la Nairobi, imepangwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kwa watazamaji kote ulimwenguni mnamo Novemba 2024.

Tamthilia Hiyo inayoitwa ‘2 ASUNDER’ imetayarishwa na Betty M. Mutua na Fakii Liwali, imeandikwa na Charles Chanchori na kuongozwa na Tony Mwaura na Fakii Liwali.

‘Trela’ la filamu hii limepangwa kutolewa siku ya Jumanne Oktoba 15, 2024, ikiambatana na matangazo yatakayotolewa kupitia kurasa za mitandao mbalimbali ya kijamii.

Muziki katika filamu hiyo umeimbwa na wasanii wenye majina makubwa nchini Kenya akiwemo Sanaipei Tande, Nyashinski, Bensoul na Alex Mugenda ‘Big Soul’.

‘2 ASUNDER’ ni hadithi ya kubuni inayomuhusu bi harusi mwenye haya nafasi ambayo imechezwa na Stephanie Ciku Muchiri na nafasi ya bwana harusi bora na katili katika filamu hii imechezwa na Kevin ‘K1’ Maina.

Waigizaji wengine walioigiza katika filamu hiyo ni DJ na mchumba jasiri nafasi iliyochezwa na Sanaipei Tande. Hadithi ya filamu hii imeficha siri nzito ambazo zinatishia kuimaliza familia moja tajiri.

Filamu hii inaelezea uchunguzi wa athari za kudumu za imani na desturi za kitamaduni kupitia mitazamo ya kifamilia na ndoa.

Lugha iliyotumika katika filamu hii ni Kiingereza na Kiloka (lugha ya kubuniwa yenye athiri za Kibantu iliyoundwa mahsusi kwa ajili ya filamu hii).

Mwaira amesema filamu hiyo ya ‘2 Asunder’ ni filamu yenye hadithi nzuri, na tumaini lake ni kwamba watazamaji watathamini jinsi hadithi hiyo inavyoeleza uhalisia wa maisha halisi.

Tony, katika muongo mmoja uliopita, ameongoza matangazo mbalimbali ya TV na video za muziki wa pop chini ya kampuni yake, Absolute Media Pictures (AMP), na hii ni mara yake ya kwanza kuingia katika uongozaji wa filamu.

Filamu hiyo imeandaliwa kwa muda mrefu na upigaji picha wake ulianza tangu Septemba 2023 ambapo siku 10 zilizotumika katika upigaji risasi katika kaunti za Nairobi na Kiambu nchini Kenya na maeneo mengine manne makuu, Marula Manor, Sovereign Suites, Tigoni na Paradise Lost.

Filamu ya ‘2 ASUNDER’ imefaidika na Mpango wa Uwezeshaji wa Filamu (mzunguko wa 3, 2023) na Tume ya Filamu ya Kenya kwa ushirikiano na Shirika la Ujerumani katika Ushirikiano wa Kimataifa. Filamu hiyo imepewa namba 18 na Bodi ya uainishaji wa filamu nchini Kenya (KFCB).

Related Articles

Back to top button