Serie A
Mtoto wa Zlatan Ibrahimovic asajiliwa AC Milan
MTOTO wa Zlatan Ibrahimovic, Maximilian, ametia saini mkataba wake wa kwanza katika soka kwa kujiunga na klabu AC Milan inayotamba huko Serie A.
Mtaalamu wa uhamisho wa kandanda, Fabrizio Romano, aliandika kwenye akurasa wake wa X kwamba Maximilian ataanza kucheza na timu ya vijana ya AC Milan ‘Milan Futuro’.
Romano aliandika; “Mtoto wa Zlatan Ibrahimović, Maximilian ametia saini mkataba wake wa kwanza wa kuwa katika klabu ya AC Milan ambayo baba yake aliwahi kuichezea.
Zlatan Ibrahimovic kwa sasa ni mshauri mkuu wa AC Milan, amewahi kuichezea klabu hiyo siku za nyuma na ataanza kucheza na timu ya vijana kama maendeleo yake yatakuwa mazuri anaweza kupandishwa timu ya wakubwa.