Kikapu

Moto wa Wasichana U16 kuendelea dhidi ya Kenya

KIBAHA PWANI: KOCHA Msaidizi wa timu ya mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball) Wasichana U 16 ya Tanzania, Nelious Mrugeni amesema ana kazi kubwa kwenye mchezo wa fainali ya kesho dhidi ya mpinzani wake Kenya.

Tanzania wanacheza fainali dhidi ya Kenya katika mashindano ya Afrika kanda ya tano, yanayoendelea katika uwanja wa ndani wa Filbert Bayi uliopo Kibaha, Pwani.

Kocha huyo ameiambia Spotileo kuwa amewaangalia wapinzani wao Kenya katika mchezo na Burundi, anaimani mechi yao ya kesho watakuja kivingine.

“Siwezi kusema tutashinda au Kenya watashinda, kazi ipo kwa sababu wapinzani wetu hawatakuja kucheza kama walivyocheza leo na hata sisi hatutacheza tulivyocheza na Burundi

“Kila mmoja atakuja na mipango yake, kikubwa tumeandaa timu kwa ajili ya kushindana na kutwaa ubingwa wa michuano hii ya Kanda ya tano,” amesema Kocha Nelious.

Mashindano hayo ya Kanda ya tano yameshirikisha timu za Afrika Mashariki Tanzania akiwa ni wenyeji wa mashindano, Kenya na Burundi ambao wamepoteza michezo yote miwili.

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button