Kikapu

Baba Levo: Hasheem ameiheshimisha Dar City

DAR ES SALAAM: MSEMAJI wa klabu ya mpira wa kikapu ya Dar City Revocatus Chipando ‘Baba Levo’ amesema uwepo wa Hasheem Thabit katika kikosi hicho kumechangia kupata ubingwa wa taifa.

Dar City ilitwaa ubingwa huo mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma baada ya kuichapa ABC kwa pointi 78-46 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana jioni baada ya timu hiyo kurejea Dar es Salaam, Baba Levo amesema hawakuwa na uwezo wa kumlipa mchezaji huyo wa kimataifa lakini alikubali kujitolea kwa nguvu zake kuisaidia timu.

“Shukrani kwa wachezaji wote kwa kujitolea, mchezaji kama Hasheem Thabit ametuheshimisha sana hatukuwa na uwezo wa kumlipa lakini kwa nguvu zake amekubali kupambana na kuisaidia timu kuleta kombe, tunamuomba sana asitutupe twende naye popote pale kuhakikisha Dar City inapeperusha bendera ya Tanzania,”amesema.

Amesema ushindi wa kombe hilo unawapa nafasi ya kujiandaa na michuano mbalimbali ya kimataifa kama mwakilishi wa nchi na wako tayari kwa vita.
Mchezaji wa Dar City Ally Abdallah amesema kilichowasaidia kushinda kila mchezo kwao walichukulia kama fainali.

Kingine alisema walikuwa na timu bora kuliko wapinzani hivyo, ana imani walipoishia kama wataandaliwa vizuri zaidi kwa ajili ya michuano ijayo ya Afrika watafanya maajabu zaidi.

Related Articles

Back to top button