Africa

Mosimane apokelewa kwa heshima Al Ahly

CAIRO: ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Al Ahly, Pitso Mosimane ametua makao makuu ya timu hiyo na kupokelewa kwa heshima kubwa.

Mosimane raia wa Afrika Kusini ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa, Bafana Bafana yupo Cairo kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Misri itakayochezwa Oktoba 4, mwaka huu na kuamua kuzuru katika klabu yake hiyo ya zamani.

Kocha huyo anakumbukwa Ahly au Red Eagles kwa mafanikio yake makubwa akiwa hapo ikiwemo kutwaa ndoo ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili mfululizo, msimu wa 2019-20 na 2020-21.

Katika kuonyesha heshima na shukrani kwa mchango wake mkubwa, uongozi wa Al Ahly umemzawadia Mosimane ngao maalum ya ukumbusho, beji ya heshima na jezi ya sasa ya timu hiyo.

“Mosimane amerejea nyumbani.
Kocha wetu gwiji ametembelea mahali ambapo aliweka historia na kuandika kurasa zisizosahaulika akiwa na Red Eagles,
Tunafurahi kukuona kila wakati, kocha,” ukurasa wa Ahly wa Mtandao wa Instagram uliweka maneno hayo na kusindikiza na baadhi ya picha za Mosimane akiwa klabuni hapo.

Aidha, Bafana Bafana ambayo imeshinda michezo yake miwili ya mwisho kuwania kushiriki AFCON 2017, itamenyana na Misri kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, uliopo jijini Cairo.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button