Burudani
Diamond aongoza mgao mwingi mirabaha Cosota

DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameongoza orodha ya wanufaika wa mgao wa tozo za mirabaha kwa kupata Sh milioni 12.2, akifuatiwa na Ali Saleh ‘Alikiba’ aliyepata Sh milioni 7.3.
Katika mgao huo uliotolewa na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania COSOTA Dar es Salaam Leo chini ya mgeni rasmi Naibu Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Methusela Ntonda Kwaya ya Mtakatifu Cecilia ya Arusha imekuwa ya tatu kwa kupata Sh milioni 6.8, huku wasanii wengine pamoja na kampuni zinazosimamia kazi za sanaa nazo zikinufaika na malipo hayo.
Mgao huo ni sehemu ya hatua ya Serikali kuhakikisha wasanii na wabunifu wananufaika na kazi zao kupitia tozo zinazokusanywa kutokana na matumizi ya kazi za sanaa.




