Mohamed Muya kocha mpya Geita

GEITA: UONGOZI wa klabu ya soka ya Geita Gold umemtangaza Mohamed Muya kutoka Fountain Gate kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo.
Muya anachukua nafasi ya Amani Josia aliyetimkia Tanzania Prisons kuchukua kuchukua mikoba ya Mbwana Makata.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Geita Gold Ramadhan Bukambu, Kocha Muya amesaini mkataba wa kuwa Kocha Mkuu wa klabu mpaka mwisho wa msimu wa NBC Championship 2024/2025 .
” Ni mtu ambaye ana uzoefu na mpira wa Tanzania tunategemea atatuongoza vyema kurejea Ligi Kuu msimu ujao,”alisema.
Muya ataendelea kufanya kazi na benchi la ufundi lilokuwepo awali huku dhamira kuu ya klabu ikiwa ni kurejea Ligu Kuu Tanzania bara msimu wa 2025/2026.
Geita inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo nyuma ya Mbeya City na Mtibwa ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza michezo 14, kushinda tisa, sare tatu na kupoteza miwili.