Ligi Daraja La Kwanza

Harmonize amwaga maua kwa Rais Samia

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Rajab Abdul ‘Harmonize’ amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutimiza ahadi yake aliyoahidi kuhusu kuwapeleka wasanii kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Harmonize amesema anamshukuru sana kwa kutimiza ahadi yake.

“Nadhani wote mnajionea na ni mashahid, kama mnavyoona Wasanii wa bongo muvi wameenda nchini Korea na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Sanaa ya maigizo.”amesema.

Pia amesema kuwa kwa wasanii huu ni wakati wa kuchangamkia fursa za kazi zao kwani mama ameshasema watumie fursa.

Wakati huo huo Msanii huyo wa Bongo fleva amejibu kuhusu kutokufika kwa msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na Zuhura Othuman ‘Zuchu’ kuhudhuria uzinduzi wa albamu yake iliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu.

Akizungumza na Spotileo jijini Dar es Salaam Harmonize amesema kuwa moyo wa mtu ni kichaka na huwezi kujuwa mtu anawaza nini.

“Kwa upande wangu nilitegemea wao kuwepo lakini hawakuja kwa sababu zao wenyewe, labda walikuwa na shughuli zao lakini kwa upande wangu nachukilia sawa.”

Related Articles

Back to top button