Mastaa

Mkwere: Nilibeba mabegi nionekane kwenye tv

MWIGIZAJI mkongwe wa vichekesho Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ amesema ametoka mbali katika sanaa na anakumbuka namna alivyobeba mabegi ya watu maarufu kwa ajili ya kupata nafasi ya kuonekana .
Akizungumza na SpotiLeo Mkwere amesema zamani mpaka mtu akitambue kipaji chako ni lazima upambane na yeye alitumia fursa ya kubeba mabegi ya watu maarufu kusudi tu ndoto zake zitimie.
 
“Hadithi yangu nikifikiria kwa kweli nimetoka mbali hadi leo najivunia mafanikio, haikuwa kazi rahisi. Nilibeba mabegi ili nipate nafasi ya kuigiza kwenye TV na nilifanikiwa,”alisema.
 
Nyota huyo amesema alifanya hayo yote sio kwa kupenda bali kuhakikisha anaonesha kipaji chake matokeo ambayo yalifanikiwa.
 
Mkwere ni miongoni mwa wasanii walioigiza kwa miaka mingi tamthilia za vichekesho za kwenye televisheni na leo amekuwa ni mmoja ya mastaa wakubwa wanaoaminiwa na wenye mikataba minono ya matangazo mbalimbali yanayomuingizia fedha.
 
Amesema alifanya hivyo, kwasababu zamani hakukuwa na simu janja kama sasa ambako wengi wanazitumia kuonesha vipaji. Mkwere amehimiza wasanii chipukizi kutolala bali watumie simu janja na mitandao ya kijamii kutangaza vipaji vyao

Related Articles

Back to top button