NEW DEL: MKE wa mcheza filamu mashuhuli nchini India Dharmendra, Hema Malini amefichua kwamba mkali wa filamu za kihindi, Dharmendra alikataa kufanya kazi yake kwa madai ya kukataa kuwa chini ya mke wake.
Kitendo hicho kilimuuliza mwanamke huyo ameamua kukieleza wazi sasa baada ya miaka mingi kuhangaika kupita alipokuwa akiangaikia kurekodi filamu yake ya ‘Dil Aashna Hai’ ya mwaka 1992.
Hema Malini alikuwa nyota katika miaka ya 1970 na 1980 lakini kufikia miaka ya 1990, lakini umaarufu wake huo haukumshangaza mumewe alimkatalia hadi akaamua kutafuta waigizaji waliokuwa wakichipukia akiwemo Shar Rukh Khan ndiye aliyecheza filamu hiyo ya ‘Dil Aashna Hai’.
Hema Malini amewahi kucheza katika filamu ya ‘Beyond the Dream Girl’, iliyoandikwa na Ram Kamal Mukherjee, ameeleza kwamba mwanzoni, alitaka kumsajili Vinod Khanna ili acheze filamu hiyo baada ya mumewe kukataa lakini Vinod naye hakuwa na muda kutokana na kubanwa na ratiba za kurekodi filamu nyingi wakati huo.
“Baadaye, nilimuuliza Amitabh Bachchan kwa ajili ya jukumu lile lile lakini huu ulikuwa wakati ambapo ‘Big B’ alikuwa kwenye mapumziko kwa hivyo hata yeye alikataa ndipo niliamua kumsajiri staa mpya Shar Rukh Khan ndiye alikuwa akichipukia wakati huo,” amesema.
Hena ameeleza kwamba baada ya mume wake kushindwa kucheza katika filamu yake maneno mengi yaliibuka wakiwafitinisha lakini lakini fitina zilishindwa kwa kuwa alifahamu mumewe alishindwa kucheza kaytika filamu yake kwa sababu kipindi hicho alikuwa na safari nyingi za Marekani nan chi nyingine kwa ajili ya kucheza filamu mbalimbali.
“Watu walisema kila aina ya mambo lakini hapakuwa na ukweli kwa hilo. Hakuweza kuhudhuria kwa sababu alikuwa Marekani kwa kazi zake lakini kila hatua nilikuwa nikimshirikisha naye alitoa ushauri, alikuwa msaada mkubwa licha ya kutokucheza katika filamu hiyo. Binti zangu pia walifurahishwa sana na filamu hii,” amefafanua.