Walioshinda Tuzo za Oscar hawa hapa, filamu ya Anora yatisha

HOLLWOOD: HAWA ndio washindi katika kategoria muhimu za Tuzo za 97 za Oscar, ambazo zilitolewa siku ya Jumapili Machi 2, 2025 huko Hollywood nchini Marekani.
Filamu ya ‘Anora’ ndio iliyoibuka gumzo katika usiku huo, ikiibuka na tuzo tano za Oscar ikiwemo: Picha Bora, Muongozaji Bora, Muigizaji Bora wa kike, Uhariri Bora wa filamu na Uchezaji Bora wa awali.
Washiriki katika filamu hiyo ya ‘Anora’ walioshinda tuzo kupitia filamu hiyo Filamu Bora ambayo ndiyo ‘Anora’ pia Mikey Madison ameibuka na tuzo ya Muigizaji Bora, Sean Baker ameibuka na tuzo ya Muigizaji Bora Asilia, Muongozaji Bora wa filamu na Mhariri Bora wa Filamu.
Filamu nyingine zilizoshinda ni ‘The Brutalist’ ambayo imetoa Muigizaji Bora ambaye ni Adrien Brody, Huku filamu ya Muigizaji Msaidizi Bora ikienda kwa Kieran Culkin kupitia filamu ya ‘A Real Pain’.
Wengine ni Muigizaji Bora Msaidizi aliyoshinda Zoe Saldana, kupitia filamu ya ‘Emilia Perez’, Skrini Bora imekwenda kwa Peter Straughan kupitia filamu ya ‘Conclave’.
Tuzo ya Filamu Bora ya Kimataifa imekwenda nchini Brazil kupitia filamu ya ‘I’m Still Here’, Tuzo ya Kipengele bora cha uhuishaji imekwenda kwa filamu ya ‘Flow’, Tuzo ya Filamu Bora ya hali halisi imekwenda kwa ‘No Other Land.
Tuzo nyingine ni Ubunifu Bora wa Mavazi imekwenda kwa Paul Tazewell, kupitia filamu ya ‘Wicked’, huku Tuzo ya Filamu Bora ya Ubunifu ikienda kwa Nathan Crowley na Lee Sanders, kupitia filamu ya ‘Wicked’
Tuzo ya Filamu Bora ya Vipodozi Bora na Mitindo ya Nywele imechukuliwa na filamu ya ‘A thing’, pia Tuzo ya Wimbo bora wa asili unakwenda kwa Clement Ducol, Camille na Jacques Audiard, kupitia filamu ya ‘El Mal’ na ‘Emilia Perez’.