Kwingineko

Messi kuagwa PSG Juni 3

Kocha Mkuu wa timu ya Paris Saint-Germain(PSG) inayojulikana kama ‘Les Parisiens’, Christophe Galtier amethibitisha kuwa Juni 3 mshambuliaji Lionel Messi atacheza mchezo wake wa mwisho akiwa na matajiri hao wa Ufaransa.

Mkataba wa Messi wa miaka miwili ‘Les Parisiens’ unamalizika msimu huu na uvumi wa hatma ya mkongwe huyo umekuwa ukijirudia kwa muda mrefu.

“Nilikuwa na fursa ya kufundisha mchezaji bora zaidi katika historia ya soka. Itakuwa mechi ya mwisho kwa Leo katika uwanja wa Princes dhidi ya Clermont,” amesema Galtier.

Messi amecheza michezo 74 PSG akifunga mabao 32 tangu alipojiunga nayo akitokea Barcelona mwaka 2021.

Habari ya kuondoka kwa Messi inakoleza uvumi kuwa huenda nyota huyo akarejea Barcelona au kutimkia Uarabuni.

 

Imeandaliwa na Alfred Kavishe

 

Related Articles

Back to top button