Kwingineko

Messi alingana na rekodi ya Klose baada ya kuizamisha Algeria

KANSAS CITY: NAHODHA wa Argentina, Lionel Messi, ameandika historia nyingine katika Kombe la Dunia baada ya kufunga hat-trick na kuifikisha timu yake kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Algeria katika mchezo wa Kundi J uliochezwa Kansas City, Marekani.

Hat-trick hiyo imemwezesha Messi kufikisha mabao 16 katika historia ya Kombe la Dunia na kulingana na rekodi ya mfungaji bora wa muda wote, Miroslav Klose.

Nyota huyo mwenye miaka 38 pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga hat-trick katika mashindano hayo.

Messi aliifungia Argentina bao la kwanza dakika ya 17 baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Rodrigo De Paul kabla ya kuongeza la pili dakika ya 60 na kukamilisha hat-trick yake dakika ya 76.

Ushindi huo umeipa Argentina mwanzo mzuri wa kampeni ya kutetea taji la Kombe la Dunia huku ukiondoa mashaka yaliyokuwa yakiizunguka timu hiyo kuhusu uwezo wake wa kuendelea kutawala soka la dunia.

Baada ya mchezo, Alexis Mac Allister alisema Messi ndiye nguzo kuu ya timu hiyo, wakati beki wa Algeria Aissa Mandi akikiri kuwa walishindwa kumzuia nyota huyo ambaye alitumia kila nafasi aliyopata kuadhibu wapinzani wake.

Argentina sasa itavaana na Austria katika mchezo wake unaofuata, huku Algeria ikitarajia kurejea uwanjani dhidi ya Jordan.

Related Articles

Back to top button