“Nina kikosi bora zaidi Duniani” – Luis Enrique

BIRMINGHAM:KOCHA mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) PSG, Luis Enrique amesema kikosi chake ni kikosi bora zaidi duniani kwa sasa baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi dhidi ya Aston Villa ya Mabingwa barani Ulaya jana kwa ushindi wa jumla (Aggregate) wa 5-4 ugani Villa Park Jumanne
Enrique ameiambia Amazon prime TV kuwa ubora wa kikosi cha PSG hauishii eneo la ulinzi pekee baada ya hapo jana golikipa wa kikosi hicho Gianluigi Donnarumma kukaa imara langoni akiokoa michomo kadhaa kipindi cha pili ambayo ingeweza kuwafanya kwenda extra time na kuiweka mashakani nafasi yao hiyo ya nusu fainali.
“Nadhani tuna kikosi bora zaidi Duniani kwa sasa, na sio golikipa pekee ukiwa kwenye klabu kama PSG lazima uwe na wachezaji wenye viwango bora. Nikiangalia vizuri naona Tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda michezo yote miwili” amesema
“Tumeanza vizuri mchezo huu, tukafunga mabao mawili mazuri sana kipindi cha kwanza. Lazima ujue hii ni Champions league na lazima ukubali ubora wa kila mpinzani, Villa wana timu nzuri sana wamecheza kwa ubora sana kipindi cha pili walijitoa kwakuwa hawakuwa na cha kupoteza” aliongeza
PSG waliotangulia kwenye nusu fainali watautazama mchezo wa Real Madrid dhidi ya Arsenal leo usiku ili kufahamu ni nani watakutana nae katika hatua hiyo ambayo ni hatua muhimu ya kusaka historia ya kutwaa kombe hilo kwa mafa ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.