Filamu

Mchina ndiye mtayarishaji filamu tajiri zaidi Asia

CHINA: MTAYARISHAJI wa filamu wa China na gwiji wa vyombo vya habari Wang Changtian ndiye mtayarishaji filamu tajiri zaidi barani Asia, kulingana na orodha ya Forbes.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 59 ana utajiri wa dola bilioni 3.5, ambao ni wa juu zaidi kuliko mwigizaji yeyote wa filamu barani Asia, wakiwemo wakali kama Jackie Chan, Shah Rukh Khan, Aditya Chopra na Karan Johar.

Utajiri wake wa dola bilioni 3.5 umewazidi matajiri wengine katika utayarishaji wa filamu akiwemo Aditya Chopra ambaye anadola milioni 900, Shah Rukh Khan anadola milioni 770 na Tom Cruise anadola milioni 800.

Wang amekuwa Tajiri hivyo kupitia kampuni yake ya vyombo vya habari, Beijing Enlight Media, kampuni inayoongoza katika utengenezaji wa filamu nchini China.

Wang Changtian alianza kama mwandishi wa habari kabla ya kuwa mtayarishaji wa redio na TV. Baada ya kupata uzoefu wa kutosha, alianzisha Beijing Enlight Media mwaka 2005, ambayo imeendelea kumtambulisha kama mmoja wa watengenezaji filamu wenye nguvu zaidi duniani.

Related Articles

Back to top button