Nyumbani

Mchango wa wanawake wajadiliwa

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao imefanya kikao na Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dk Dorothy Gwajima kutambua mchango wa mwanamke.

Dk Gwajima amesema kikao hicho kinalenga kutambua umuhimu wa wanawake hasa kulinda utamaduni wetu na kukikumbusha kizazi hichi kulinda amani na kukemea vitendo vya ukatili na kuvunja utu.

Ameahidi kutoa ushirikiano baina ya Wizara yake na Taasisi ya Mama ongea na mwanao na wanatambua mchango wao.

Kwa upande wake Steve Nyerere amesema Mama ongea na mwanao wanatarajia kuanzia kampeni ya Samia nivishe kiatu, baiskeli ya mama na makundi ya walemavu.

Aidha amesema Kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani mwezi wa tatu wanaamini taasisi ya hiyo  itatoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha jambo la mama ni jambo letu.

Related Articles

Back to top button