Mayele: Tulimuhofia Msuva, Samatta

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya DR Congo, Fiston Mayele ameshangazwa kutomuona winga Simon Msuva katika kikosi cha Taifa Stars, akisema kuwa walikuwa wakiuwaza mziki wake walipokuwa uwanja wa mazoezi.
Mayele amesema katika maandalizi ya mechi yao dhidi ya Taifa Stars mpango wao mkubwa ilikuwa ni kuweka ulinzi kwa Mbwana Samatta na Msuva lakini kutomuona nyota huyo ikawa nafuu kwao.
“Kati ya wachezaji tuliowahofia na kuwafanyia mikakati mikubwa katika uchezaji ni Samatta na Msuva lakini imetushangaza kutomuona nyota huyo imekuwa nafuu kwetu maana tuliamini wachezaji hao ndio wasumbufu na injini ya Stars” amesema Mayele.
Amesema walijiandaa vizuri wana wachezaji wazuri watanzania wanapaswa kufahamu Msuva alikuwa hatari, kocha Sebastiaen Serge alimuulizia Msuva kama kaitwa kikosini.
“Wawili hao wanapokuwa katika timu mara nyingi tunakuwa na hofu, kocha ameshangaa kutomuona Msuva, licha ya Samatta kucheza vizuri,” amesema Mayele.