AFCONAfrica

Diarra, Aziz Ki AFCON leo

TIMU za Mali na Burkina Faso waliopo wachezaji wa Yanga golikipa Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki zinashuka viwanja tofauti leo katika mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea Ivory Coast.

Burkina Faso itaikabili Mauritania katika mchezo wa awali kundi D utakaofanyika uwanja wa La Paix uliopo mji wa Bouaké.

Katika mchezo utakaofuatia wa kundi D, Tunisia itaavana na Namibia kwenye uwanja wa Amadou Gon Coulibaly uliopo mji wa Korhogo.

Mechi ya mwisho na ya kukata na shoka ya kundi D itazikutanisha Mali na Afrika Kusini kundi itakayofanyika kwenye uwanja huo huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button